TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI, HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA 08-07-2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi
wote walioomba kazi ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II, Katibu Mahsusi
Daraja III na Dereva wa Mitambo Daraja II kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa
kuanzia tarehe 15 hadi 21 Julai, 2020.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Ratiba ya usaili imeonyeshwa kwenye jedwali hapo chini;
ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa
Barakoa (Mask) na kuzingatia maelekezo yote ya kujikinga na
Corona;
iii. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na; Kitambulisho cha Mkazi,
Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha Kazi, Kitambulisho cha
Uraia au Hati ya Kusafiria;
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa, kidato cha IV au VI, Astashahada na “Transcript”.
vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV au VI (form V and
form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA
KUENDELEA NA USAILI;
vii. Kila Msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
viii. Kwa Waombaji kazi waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU , NACTE na
NECTA);
ix. Kila Msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
x. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika ambaye ni NECTA.
xi. Orodha ya Waombaji kazi walioitwa kwenye usaili inapatikana kwenye
tovuti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambayo ni www.dodomacc.go.tz ,
na mbao za matangazo za Halmashauri.
xii. Tahadhari usaili utafanyika kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za
Utumishi wa Umma, kuna matapeli wanaotumia majina ya watu na vyeo
vya watu kwa lengo la kujipatia fedha kuweni makini na matapeli hao.
xiii. Waombaji kazi ambao majina yao haya kuonekana katika tangazo hili
watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi
nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

 

 

MAJINA // TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI