TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI TRA 24-06-2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba
kazi kuwa usaili wa mchujo unatarajiwa kufanyika tarehe 4 Julai, 2020 na kufuatiwa
na usaili wa mahojiano ambao tarehe itapangwa baadae.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili wa mchujo utafanyika tarehe 04 Julai, 2020 kama ilivyooneshwa
kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika
umeainishwa kwa kila Kada;
ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa
Barakoa (Mask) na kuzingatia masharti mengine ya kujikinga na
COVID 19 KAMA YALIVYOAINISHWA NA WIZARA YA AFYA awapo
eneo la usaili,
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na ama Kitambulisho cha Mkazi,
Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi cha taasisi
inayojulikana, Kitambulisho cha Uraia ,Hati ya kusafiria au Leseni ya
Udereva
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada
na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V
and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA
KUENDELEA NA USAILI;
vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA, NACTE au
TCU);
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayaonekani katika tangazo hili
watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi
nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma
wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za
kufanyia kazi.

 

MAJINA // TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI