KUITWA KWENYE USAILI BUSEGA DC 24-06-2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI.

Kutokana na Tangazo la nafasi za kazi lenye Kumb.Na. BDC/C.30/17/58 la tarehe 06 Mei,
2020 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega anatarajia kuendesha
Usaili na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji watakao faulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa wazingatie mambo Muhimu yafuatayo;
• Usaili utafanyika tarehe 08 Julai,2020 kuanzia saa 2:30 Asubuhi Usaili wa
mchujo/Vitendo na tarehe 09 Julai, 2020 Usaili wa mahojiano (kwa watakaofanikiwa)
katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Nyashimo.
• Ukaguzi wa vyeti utaanza saa 1:30 asubuhi kabla ya muda wa mtihani wa
mchujo/usaili wa vitendo kuanza.
• Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Mfano, Kitambulisho cha mkazi, kupiga
kura, kazi, Hati ya kusafiria n.k.
• Kuja na vyeti HALISI (Original Certificates) na HALALI vya kuanzia kidato cha Nne,
Sita, Astashahada, Stashahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
• Kuja na Cheti Halisi cha kuzaliwa (ORIGINAL BIRTH CERTIFICATE).
• Testimonials “Provisional Results”, “Statement of Results” Hati ya matokeo ya
kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI) HA VITAKUBALIKA.
• Kila Msailiwa Atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
• Kwa waombaji ambao majina yao hayakuonekana katika Tangazo hili, watambue kuwa
maombi yao hayakufanikiwa na wasisiste kuomba tena mara nafasi za kazi
zitakapotangazwa

 

MAJINA // TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI