TANGAZO LA KUITWA KAZINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na. EA.7/96/01/K/226 30 JUNI, 2020

TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu Waombaji
Kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 20 – 22 Mei, 2020 na tarehe
08 – 17 Juni, 2020 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni
kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia
inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa
kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi
kupatikana.
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha
kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo
Barabara ya Kivukoni, Jengo la Utumishi, Masjala ya Wazi ndani ya siku
saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo
hazijachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi
wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye
2
barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals
Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili
vihakikiwe na Mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa
hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine
nafasi za kazi zitakapotangazwa.

 

MAJINA // TANGAZO LA KUITWA KAZINI