TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA MOROGORO

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro anapenda kuwatangazia
waombaji wote walioomba kazi ya Mtendaji wa Mtaa Daraja III kuwa Usaili utafanyika
tarehe 20 na 23 Juni, 2020 saa 1:00 asubuhi katika Chuo Kikuu Jordan (HEKIMA
HALL).
Aidha Usaili wa Mchujo (Written Interview) utafanyika tarehe 20/06/2020 na
wasailiwa watakaofaulu ndio watakaochaguliwa kuendelea na Usaili wa Mahojiano
(Oral Interview) tarehe 23/06/2020 katika Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro siku ya
Jumanne kuanzia saa 1:00 Asubuhi.
Orodha ya waombaji walioitwa kwenye usaili ni kama inavyoonekana hapo chini, kwa
waombaji ambao majina yao hayakuonekana katika orodha hiyo watambue kuwa
maombi yao hayajakidhi sifa kwa mujibu wa nafasi zilizotangazwa. Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro anawashukuru kwa kuleta maombi ya kazi
na wasisite kutuma maombi tena kipindi Halmashauri itakapotangaza nafasi za kazi
ambazo zitaendana na sifa walionazo.
Waombaji wote walioitwa kwenye usaili wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-

i. Wasailiwa wafike na Vyeti Halisi (Original) vya Taaluma, Kuzaliwa, Vyeti vya
Shule na Kitambulisho.

ii. Vitambulisho vitakavyokubaliwa ni pamoja na Kitambulisho cha Uraia,
kitambulisho cha Kupiga Kura, Leseni ya Udereva au Pasi ya Kusafiria.
2

iii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na
NECTA).

iv. Msailiwa anayekuja kufanya usaili atajigharamia mwenyewe

v. Msailiwa anatakiwa kuzingatia tarehe, muda na eneo la usaili

vi. Usaili utafanyika kwa njia ya maandishi na mahojiano

vii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa
Barakoa (Mask) na kuzingatia maelekezo yote ya kujikinga na Corona.

viii. Tahadhari usaili utafanyika kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni za
Utumishi wa Umma, kuna matapeli wanaotumia majina ya watu na vyeo vya
watu kwa lengo la kujipatia fedha kuweni makini na matapeli hao. OFISI

HAITAWASILIANA NA MSAILIWA YEYOTE KWA NJIA YA SIMU

 

MAJINA // TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI