Tuesday, January 27, 2026
spot_img

Wanafunzi 698 washinda rufaa na kupangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 2.46 bilioni

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya majina 698 ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliofanikiwa kupata mikopo katika dirisha la rufaa kufuatia kukosa au kupata kiwango kidogo cha mkopo katika awamu nne zilizopita.

Wanafunzi hao 698 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 2.46 bilioni na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo hadi sasa kufikia 49,485. Taarifa ya kina kuhusu utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 itatolewa baada ya uchambuzi wa mwisho kukamilika.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema hayo (Jumamosi, Desemba 7, 2019) jijini Dar es salaam kuwa taarifa zaidi kuhusu viwango walivopangiwa zinapatikana katika akaunti zao binafsi walizotumia kuomba mkopo – Student’s Individual Permanent Account (SIPA) kupitia httpsss://olas.heslb.go.tz

“Tumeshaweka taarifa za hawa wanafunzi katika mfumo na hivyo kila mmoja anatakiwa aingie katika akaunti yake ya SIPA ambapo ataona taarifa zake ambazo pia zinatumwa vyuoni,” amesema Badru.

Kwa mujibu wa Badru, HESLB imeboresha mifumo yake na hivyo wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza walioomba mikopo wanaweza kuona taarifa zao kutoka popote walipo kwa kutumia simu zenye mtandao wa intaneti (simu janja).

Taarifa hii pia inapatikana kwenye mitandao ya kijamii na tovuti ya HESLB ambayo ni www.heslb.go.tz

 

Imetolewa na:

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Hot this week

NGAZI NA VIWANGO VYA MISHAHARA SERIKALINI | Public Servant Salary Scales – Tanzania

In 2014 , the Government implemented new Salary Scales,...

Community Growth Manager- Remote

Responsibilities We are seeking passionate, dedicated people to join as Community...

PROCEDURES AND REQUIREMENTS ON HOW TO GET TANZANIA PASSPORTS AND TRAVEL DOCUMENTS

Tanzania government issues various types of passports and other...

UNIVERSITY OF EDINBURGH JULIUS NYERERE MASTERS SCHOLARSHIPS 2025 FOR TANZANIANS TO STUDY IN THE UK (FUNDED)

Application Deadline:  28th January 2025.  Applications are now open for the...

Retail Sales Associate – Adidas

Full job description   RETAIL SALES ASSOCIATE Department: Retail Operations Direct Reporting Line:...

Digital Sales Representative required in South Africa

Full job description Job Overview Date Posted: Posted 7 days...

General Assistant – ADvTECH

Full job description The ADvTECH Schools Division leads the private...

MARKETING AND COMMUNITATIONS MANAGER, LALIGA SOUTH AFRICA (3363)

Full job description Are you interested in developing an international...

Central Data Capturer – Centurion – Ampath Laboratories

Full job description Advert Reference: P13870 Central Data Capturer - Centurion Job...

Apprenticeship (x40) – Afgri South Africa

Full job description AFGRI is offering an opportunity for an...
spot_img

Related Articles

Popular Categories

spot_imgspot_img