TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MNH STAMICO TARI TIRA TPRI TCAA MDAs &; LGAs

 OFISI YA RAIS 

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/217 12 Juni, 2020

 

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Muhimbili
National Hospital (MNH), State Mining Corporation (STAMICO), Tanzania
Agricultural Research Institute (TARI), Tanzania Insurance Regulatory Authority
(TIRA), Tropical Pesticides Research Institute (TPRI), Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA) na MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote
walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 18 hadi 26 Juni,
2020 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi Waombaji Kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 18 hadi 26 Juni, 2020 kama ilivyooneshwa
kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa
kwa kila Kada;

ii. Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa Mchujo na
na kwa wale wenye Vitendo pia watafanya hivyo wakipita hatua ya awali, namba
hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombi ya
kazi wa Sekretarieti ya Ajira.

iii. Kila Msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa
Barakoa (Mask);

iv. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
2

v. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi,
Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au
Hati ya kusafiria;

vi. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na
kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vii. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and
form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA
KUENDELEA NAUSAILI;

viii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;

ix. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

x. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE au NECTA);

xi. Waombaji kazi ambao majina yao haya kuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi
zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

xii. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma
wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za
kufanyia kazi

 

 

MAJINA // TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

MAJINA // TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI 2