PSLE 2020 EXAM TIMETABLE (RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2020)

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PRIMARY SCHOOL LEAVING EXAMINATION TIMETABLE) SEPTEMBA, 2020

 

MAELEKEZO MUHIMU

1. Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Mtihani ya mwaka 2020 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.

2. Kabla ya kufungua bahasha yoyote yenye maswali ya Mtihani, hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kujihakikishia kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Mtihani.

3. Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo ndani ya Karatasi ya Mtihani na Ratiba ya Mtihani, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya Mtihani husika ndiyo yatakayofuatwa.

4. Watahiniwa WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa Mtihani wa Kiswahili, ‘English Language’, Maarifa ya Jamii na Sayansi.

5. Watahiniwa WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa mtihani wa Hisabati.

6. Msimamizi wa watahiniwa WASIOONA awe mtaalamu mwaminifu aliye na uwezo wa kusoma maandishi na alama za ‘Braille’.

7. Watahiniwa wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za mtihani na za kujibia zenye maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.

8. Karatasi zenye majibu ya watahiniwa wenye UONI HAFIFU zifungwe kwenye bahasha za pekee. Zisichanganywe na karatasi za watahiniwa wenye Uoni wa kawaida.

9. Watahiniwa waelekezwe;

(a) Kuingia ndani ya chumba cha mtihani nusu saa kabla ya muda wa mtihani na watakaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya mtihani kuanza hawataruhusiwa.

(b) Kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa mtihani.

(c) Kuandika namba ya mtihani kwa usahihi.

(d) Kutofanya mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina ya watahiniwa. Ikiwa mtahiniwa ana tatizo anatakiwa kunyosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa mtihani.

(e) Watakaojihusisha katika udanganyifu watafutiwa matokeo yao ya mtihani.

 

BONYEZA HAPA KUONA RATIBA KAMILI

Total
0
Shares
1 comment

Comments are closed.

Previous Article
US embassy Tanzania

Department of State-Embassy of the United States, Dar es Salaam, Tanzania : Notice of Funding Opportunity (NOFO)

Next Article

ACSEE 2020 EXAM TIMETABLE (RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA SEKONDARI YA JUU 2020)

Related Posts