TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALIMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA 06-07-2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/ K/230                                                              06,Julai, 2020

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, anakaribisha maombi ya kazi kutoka
kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi nne (04) kama ilivyoainishwa
hapa chini.

1. MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II – NAFASI 04

1.1MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandika na kutunza register zinazohusu shughuli za uhasibu;
ii. Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha;
iii. Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu;
iv. Kupeleka barua /nyaraka za uhasibu Benki;
v. Kufanya usuluhisho wa masurufu,karadha,Hesabu za Benki na Amana;
vi. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa
kazi.

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
2
Kuajiriwa wenye cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka chuo
kinachotambulika na Serikali au cheti cha ATEC level I kinachotolewa na NBAA,
au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA.

1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali TGS. B.

MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa Waajiri wao.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya Wadhamini
(referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
– Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
– Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
– Computer Certificate
– Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
– Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
viii. Waombaji wa nafasi za Ajira waliostaafishwa/kuachishwa kazi katika Utumishi wa
Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
3
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni Waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Julai, 2020
xii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo;
httpss://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia
sehemu iliyoandikwa ‘RecruitmentPortal’)