TANGAZO LA NAFASI YA KAZI LITA 10-07-2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/K/239                                                                         10 Julai, 2020

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wakala wa
Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ya kazi moja (1) kama
ilivyoainishwa hapa chini.

1. MKUFUNZI MIFUGO DARAJA LA II- NAFASI 1

1.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo;
ii. Kuandaa mtiririko wa kila somo (Lesson plan) kwa upande wa nadharia na
vitendo;
iii. Kufundisha kozi za stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na
vitendo;
iv. Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza;
v. Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao;
2
vi. Kupima maendeleo ya wanafunzi kwa kushirikiana na maofisa mifugo wa wilaya,
viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practicals);
vii. Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakavyopangiwana na mkuu wake;
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali au sifa
inayolingana nayo.

1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali TGS.D

MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi
kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya Wadhamini
(referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo ngazi mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
– Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates,
– Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI,
– Computer Certificate,
– Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards),
– Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Hakikisha nakala ya vyeti vya kitaaluma pamoja na cheti cha kuzaliwa unavyoviweka
kwenye mfumo wa maombi ya kazi vimethibitishwa na Mwanasheria aliyeidhinishwa.
3
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA
xiii. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa iliyoandikwa kwa
Kiswahili au Kiingereza na barua hiyo ielekezwe kwa Katibu, Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bararaba ya 8, Kivukoni S.L.P
63100 Dar Es Salaam.
xiv. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 23 Julai, 2020.
xv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo;- httpss://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Limetolewa na:

KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA